Connect with us

Makala

Itakuwaje Salah Akikosekana Liverpool??

Liverpool ni timu inayoongoza Ligi Kuu England kwa sasa ikiwa imecheza mechi 29 na kujikusanyia pointi 82,japo kwa sasa ipo kwenye hatihati ya kumkosa mshambuliaji wao Mohamed Salah raia wa Misri kwa muda wa miezi minne ya msimu ujao.

Jambo hili l inakuja kutokana na kuvurugika kwa ratiba za michuano mingi ya kimataifa kutokana na kuenea kwa virusi vya Corona ambapo michuano mingi ya kimataifa imebadili ratiba zao ikiwa ni pamoja na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Jurgen Klopp ambaye ni kocha mkuu wa Liverpool tayari ameanza kupasua Kichwa kujua ni nani atakayekuwa mbadala wa Salah iwapo mambo yatakuwa ndivyo sivyo.

Kocha wa timu ya Taifa ya Misri chini ya miaka 23, Shawky Gharib amesema kuwa mchezaji Salah ana uwezo wa kipekee na kila kocha ambaye anafanya naye kazi ni lazima ampe nafasi ndani ya kikosi chake kutokana na uwezo aliokuwa nao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala