Connect with us

Makala

Mzambia Kuwapasua Kichwa Simba

Mshambuliaji anayekipiga ndani ya klabu ya Orlando Pirates,Justine Shonga  bado yupo kwenye vichwa vya mabosi wa Simba wanaotaka kuipata saini yake huku kinachowapasua kichwa ni dau lililowekwa mezani.

Shonga mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na klabu ya Orlando Pirates akitokea Nkwazi FC ya Zambia mwaka 2017 kwa dau la milioni 383, huku ndani ya timu ya Taifa ya Zambia ana nafasi kwani tangu mwaka 2017 mpaka sasa tayari amecheza jumla ya mechi 24 na kutupia mabao 13.

 

Mabosi wa Simba wana hamu kubwa ya kumpata nyota huyo licha ya pesa inayohitajika kuanzia shilingi milioni 800, pia upo uwezekano wa kupungua na kumnyakua mwamba huyo ndio maana mazungumzo yanaendelea.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala