Connect with us

Makala

Chama Akanusha Yasemayo Mitandaoni

Kiungo wa Simba Sc,Clatous Chama amesema kuwa amesikia yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu yeye kuwa amewakaushia mabosi wake kuhusu mkataba mpya lakini yote si ya kweli na wanayoyazungumza hayana ukweli wowote.

Mzambia huyo amesema sio kweli kuwa amekataa kusaini mkataba upya ila suala la ugonjwa wa virusi vya Corona ndio uliotibua kwani limesimamisha hata ligi kuu na kwa sasa yupo nchini kwao Zambia akizidi kujikinga dhidi ya ugonjwa huo hatari.

“Si kweli kama inavyosemekana nimekataa kusaini upya mkataba Simba ,hayo ni maneno ya watu tu na nichoweza kusema msubiri wakati sahihi utakapofika kwani kwa sasa nipo mapumziko nikijifua kivyangu ili kulinda kiwango changu”alisema Chama

Chama tangu atue msimbazi  miaka miwili iliyopita amekuwa mmoja wa mhimili wa timu hiyo hasa kazi kubwa aliyofanya na wenzake kuifikisha Simba robo fainali mbali na kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara kwa misimu miwili mfululizo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala