Connect with us

Soka

Afisa Habari Simba sc Afariki

Aliyewahi kuwa msemaji wa klabu ya Simba sc Asha Muhaji amefariki dunia leo kwa ugonjwa wa homa ya mapafu baada ya kulazwa kwa muda mrefu katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam.

Asha ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe nchini hasa kwa wanawake amefariki leo mchana huku taarifa zaidi zikisubiriwa baada ya kikao cha familia kumalizika.

Msiba huo ni pigo kubwa kwa timu ya Simba ambapo marehemu alikua mwanachama wa timu hiyo huku akiwa bega kwa bega na timu ya wanawake ya klabu hiyo Simba queens.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka