Connect with us

Makala

Aliyekuwa Rais Wa Madrid Afariki

Rais wa zamani wa timu ya Real Madrid ya Hispania, Lorenzo Sanz amefariki dunia kwa virusi vya corona akiwa na umri wa miaka 76.

Sanz amekuwa akiitumikia timu ya Real Madrid kwa kipindi cha miaka mitano (1995 – 2000) na alipoteza maisha jana wakati akipatiwa matibabu ya virusi vya Corona.

Akiwa madarakani 1998 alifanikisha timu yake ya Madrid kucheza fainali ya kwanza ya michuano ya Ulaya na hata kushinda kombe la ligi ya mabingwa ulaya mara mbili.

Kupitia ukurasa wa twitter mwanaye alisema”Baba yangu amefariki huu ndio mwisho wake kwa sasa, amekuwa kiongozi mzuri na mtu ambaye nimekuwa nikimfuata katika mengi, alikuwa ni mchapakakazi na ni miongoni mwa watu ambao sijawahi kuwaona”.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala