Connect with us

Makala

Raisi Tff ,Stop Kuvuka Mpakani

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia amesema kuwa wachezaji wote wa kigeni wanaotumika ndani ya Tanzania iwapo wataondoka nchini hawataruhusiwa kurudi tena nchini kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona.

Karia amesema kuwa ligi kuu bara imesimamishwa na serikali ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari kwa ajili ya virusi vya Corona hivyo wanaondoka na kwenda nje ya nchi huko hawatambui aina ya maambukiza yapo kwa kiasi gani.

“Hawajapewa likizo wachezaji bali ligi imesimama kwa ajili ya tahadhari ambayo inachukuliwa kwa sasa endapo wachezaji wa kigeni watakwenda kwenye nchi zao katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama hawataruhusiwa kushiriki ligi ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona”

“Tahadhari kuchukuliwa ni muda wote na sio mda mfupi hivyo tutawasiliana na mamlaka husika ili kuona namna gani tutawazuia na hawataweza kushiriki kwenye ligi iwapo hali itatulia”alisema Karia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala