Connect with us

Makala

Sababu Ya Kutokufika Kambini,Mkude

Jonas Mkude ambaye ni winga wa Simba  ameeleza sababu kubwa iliyomfanya ashindwe kujiunga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ni matatizo ya kibinadamu yanayomkabili na siyo suala la utovu wa nidhamu.

Nyota huyo alichelewa kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyokuwa imeweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na michuano ya CHAN iliyotarajiwa kufanyika nchini Cameroon  kabla haijaahirishwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Coronavilivyoingia duniani.

“Haina maana kwamba mimi ni mtovu wa nidhamu ndio maana nilichelewa kujiunga na timu ya Taifa hapana ninaithamini kazi yangu lakini masuala ya kibinadamu ndiyo ambayo yamekuwa yakinitatiza na kushindwa kuwahi kwenye kambi”alisema Mkude

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala