Connect with us

Soka

Licha Ya Corona,Stars Kambini

Rais wa shirikisho la soka Tanzania(Tff) Wallace Karia amesema kuwa kambi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) itaendelea kama jinsi ilivyopangwa na shirikisho hilo.

Karia amesema hayo kufuatia kuibuka kwa sintofahamu kuhusu kambi hiyo baada ya mechi ya kufuzu michuano ya Afcon 2021 nchini Cameroon ambapo Taifa Stars ilibidi icheze na Tunisia kughairishwa na shirikisho la soka barani Afrika(Caf) kwa hofu ya maambukizi ya virusi vya Corona.

“Barua ya CAf imeeleza kwamba, mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani ‘CHAN’ yatatolewa maamuzi baada ya kamati maalumu iliyotumwa Cameroon kuleta jmajibu juu ya usalama kuhusiana na Corona”

“ hivyo kambi ya timu ya Taifa itaendelea kama kawaida kwa ajili ya wachezaji wa ndani kupata nafasi ya kuendelea kujiandaa kwa lolote litakalo amuliwa “ Alisema Rais Karia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka