Connect with us

Makala

United Yaitengenezea Daraja Liverpool

Ushindi walioupata Manchester United wa maba 2-0 dhidi ya Manchester City umeitengenezea nafasi kubwa Liverpool ya kutwaa ubingwa kwani atakuwa na mechi mbili tu ili kutanga ubingwa wake wa kwanza ligi kuu England baada ya miaka 30.

Mchezo huo ulisimamiwa na refa kutoka England Mike Dean katika uwanja wa Old Trafford siku ya jana ,saa 1:00 usiku.

Manchester United walitoa bao la kwanza kupitia Anthony Martial dakika ya 30 huku dakika ya 90 kabla ya kipenga kulia Scott Mc Tominay aliongeza bao la pili.

Manchester City inapoteza ubora wake wa kuwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 ikifungwa na Manchester United ambayo ipo nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu England yenye pointi 45.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala