Connect with us

Soka

Barca Wamekaa Bernabeu

Timu ya soka ya Barcelona jana ilikubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania uliofanyika katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mabao ya kinda Vinicious Junior 71’na Mariano Diaz  90+2′ yalitosha kumhakikishia kocha Zinedine Zidane kuondoka na pointi tatu na kukaa juu ya msimamo kwa pointi moja zaidi ya wapinzani wao.

Vinicious anakua mchezaji mdogo zaidi kufunga bao katika mechi baina ya miamba hiyo akivunja rekodi iliyowekwa na Lionel Messi mwaka 2007 huku Mariano hapo jana ndio alicheza mchezo wake wa kwanza wa La liga msimu huu na kufanikiwa kupata bao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka