Connect with us

Makala

Club Brugge Walizwa Tena Na United

Manchester United imeamua kuweka rekodi nzuri tena mbele ya Club Brugge baada ya hapo awali kuwachapa mabao 6-1, jana wameweza kuwalaza kifo cha mende kwa kuwapiga tena mabao 5-0 katika uwanja wa Old Trafford.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 27 kupitia Bruno Fernandes ,dakika ya 34 Odion Ighalo alijipatia bao la pili huku kabla ya kwenda mapumziko ya kipindi cha kwanza cha mchezo Scott Mc Tominay alipiga bao la tatu dakika ya 41.

Fred aliwapatia furaha kubwa mashabiki baada ya kufunga bao la nne dakika ya 82 na dakika ya 90 kabla ya kipenga kulia alikamilisha bao la tano.

Msimamo wa ligi kuu unaipa Manchester United nafasi ya 5 ikiwa na pointi 41 katika mechi 27 alizocheza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala