Connect with us

Makala

Hajji Arejea Mbao Fc Kama Kocha Mkuu

Aliyekuwa kocha msaidizi wa Mbao Fc ,Abdulmutik Hajji amepewa nafasi na bodi ya Mbao Fc kuinoa timu hiyo kama kocha mkuu ili kusaidia kikosi hicho kufikia malengo hasa katika msimu huu wa ligi kuu.

Hapo awali kocha Hajji ambaye alikuwa msaidizi na bosi wake Hemedd Morroco wote waliamua kuondoka katika kikosi hicho kutokana na ubovu wa timu hiyo na madai ya kutokulipwa stahiki zao kama walivyokubaliana.

Mbao kwa sasa ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 22 imecheza mechi 23 imeshinda mechi tano kazi yake kubwa  ya Hajji itakuwa ni kuinusuru timu hiyo kushuka daraja kutokana na nafasi iliyopo kwa sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala