Connect with us

Makala

Mechi Tano Za Series A Kukosa Mashabiki

Imekuwa ni janga kubwa baada ya kusambaa kwa virusi vya Corona nchini Italia na kusababisha mechi tano za series A ikiwemo Juventus dhidi ya Intermilan kuchezwa bila ya mashabiki.

Serikali ya Italia imewazuia wakazi wa miji ya kaskazini kutembea baada ya watu takribani 229 kupatikana na virusi hivyo huku watu saba wakiwa wamekufa.

Ratiba ya mechi tano za series A zitakazochezwa bila mashabiki siku ya Jumapili ni Juventus vs Inter,Ac Milan vs Genoa,Parma vs Spal na Sassuolo vs Brescia, huku jumamosi ni Udinese vs Fiorentina.

Hii ni baada ya kuharishwa kwa mechi zao kutokana na kusambaa kwa virusi vya Corona nchini humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala