Connect with us

Soka

Fernandes Aing’arisha Man Utd

Kiungo mpya wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes ameendelea kung’ara katika kikosi cha timu hiyo baada ya jana kuisaidia kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Watford katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

Bruno alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza la Epl kwa penati dakika ya 42 baada ya Golikipa wa Watford kumuangusha ndani ya mita 18.

Pia kiungo huyo alifanikiwa kuweka assisti yake ya pili na tatu baada ya kumpa pasi Antonio Martial aliyefunga bao la pili na Mason Greenwood aliyefunga la tatu.

Man united imefikisha pointi 41 nyuma ya Chelsea iliyo nafasi ya nne huku Liverpool wakiwa kileleni mwa msimamo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka