Connect with us

Soka

Prisons Wapewa za Mezani

Timu ya Tanzania Prisons imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kwenye mchezo uliokuwa ufanyike Februari 11, 2020 baada ya Ruvu Shooting ambayo ndiyo timu mwenyeji kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance) uwanjani.

Taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka (TFF) imeeleza kuwa uamuzi huo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14 (2l) jambo lililosababisha mchezo kuvunjwa na mwamuzi baada ya kusubiri kwa dakika 30 bila gari hiyo kutokea.

Kwa mujibu wa baadhi ya waliokuwepo uwanjani siku hiyo, gari hiyo ya wagonjwa ilifika saa 10:34 (ikiwa ni dakika 4 baada ya kusubiriwa kwa nusu saa kwa mujibu wa kanuni).

Cc:AzamTv

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka