Connect with us

Soka

Sven,Eymael Wapewa Kibano

Kocha wa Simba Sven Vanden Broeck amepewa Onyo Kali kwa kosa la kugoma kuwafungulia mlango mwamuzi na Kamishina wa mchezo wakati wa ukaguzi wa timu katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 01,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.Maamuzi ya Kikao cha Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichokaa Februari 10,2020.

Kikao cha ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichokaa Februari 10,2020 Kimeielekeza Sekretarieti kufuatilia viongozi wa vilabu na Makocha ambao hivi karibuni wamekuwa wakishutumu na kutoa matamshi yenye kukashifu na kudhalilisha viongozi ,Chapa (Brand) ya Ligi na Taasisi kwa ujumla kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa vipindi tofauti tofauti.

Viongozi na Makocha waliobainika ni wafuatao Kocha wa Klabu ya Namungo FC(Hitimana )-kwenye mchezo wa Simba SC na Namungo Fc, Kocha wa Klabu ya Young African Sc (Luc Aymael)-kwenye mchezo wa Yanga Sc na Lipuli, Msemaji wa Klabu ya Simba SC (Haji Manara) na Muhamasishaji wa Young African sc(Anthonio Nugaz) .
Kutokana na matamshi hayo wanapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka