Connect with us

Soka

Fifa Yaipiga Nyundo Kaizer Chiefs

Shirikisho la soka duniani(Fifa) limeipa adhabu ya kutosajili mchezaji yeyote klabu ya Kaizer Chiefs inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika ya kusini kwa madirisha mawili mfulululizo ya usajili.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya kumsajili kimakosa mchezaji Andriamirado Andrianarimanana mwaka 2018 ambaye alikua ana mkataba na klabu ya Fosa Junior ya nchini Madagascar.

Awali Kaizer ilishinda kesi baada ya klabu ya Fosa Junior kushtaki Fifa kutokana na Kaizer kumsajili mchezaji huyo aliyekua na mkataba na Fosa lakini baada ya kupitia shauri hilo kwa kina Fifa imejiridhisha kuwa Kaizer Chiefs imefanya makosa na kutoa adhabu hiyo.

Pia mchezaji Andriamirado Andrianarimanana naye amefungiwa kujihusisha na soka kwa miezi minne huku Kaizer Chiefs wakiwa na siku 21 za kukata rufaa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka