Connect with us

Soka

Tariq Seif Arejea

Staa wa klabu ya Yanga aliyekua anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja Tariq Seif Kiakala amerejea mazoezini kujiunga na wenzake kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.

Straika huyo aliyeumia katika mechi dhidi ya Biashara united uwanja wa taifa tayari yupo fiti baada ya kufanya mazoezi kwa siku kadhaa na sasa ni suala la mwalimu Luc Eymael kumpanga tu.

“Nitakuwa tayari kuisaidia timu yangu mwalimu akinipa nafasi, naamini kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo nitakapokuwa fiti zaidi,” alisema Tariq ambaye alijiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka