Connect with us

Soka

TPLB Yawashukia Waamuzi

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 03, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 150: Simba SC 3 v Namungo FC 2-Mwamuzi msaidizi namba mbili Kassim Safisha amefungiwa miaka mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea katika mechi hiyo.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39(1)(a) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Mechi namba 157: Azam FC 1 v Mtibwa FC 1-Mwamuzi Meshack Suda ameandikiwa barua ya kukumbushwa kufanya majukumu yake kwa umakini zaidi katika mechi iliyochezwa Januari 30,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Vile vile katika mchezo huo Kamishina Abdallah Zongo ameondolewa kwenye orodha ya Makamishina kwa kosa la kutoa taarifa yenye mapungufu.Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 40(1) kuhusu Udhibiti Kamishina

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka