Connect with us

Makala

Kocha United Ampa Mwezi Mmoja Nyota Mpya

Quique Sanchez ambaye aliyekuwa kocha mkuu wa nyota mpya wa Manchester United Idion Ighalo amesema kuwa itamchukua muda wa mwezi mmoja mchezaji huyo kufikia mafanikio anayoyafikiria ndani ya Ligi Kuu England.

Sanchez alikuwa kocha wa Odion wakati akikipiga ndani ya Klabu ya Watford na raia huyo wa Nigeria alitupia jumla ya mabao 17 ndani ya msimu alipokuwa akikipiga ndani ya klabu ya Shanghai Shenua ya China kwa muda mfupi aliokuwa hapo.

“Tatizo ni kwamba mafundisho aliyokuwa anayapata ndani ya ligi ya China hayaendani na ligi ya England jambo ambalo linamfanya awe kwenye wakati mgumu kwenye mechi zake za mwanzo atahitaji muda wa mwezi mmoja kurejea kwenye ubora kwani uwezo anao ndani ya uwanja na mwili wake ulivyo atafanya mambo makubwa,” alisema

Manchester United ina matumaini makubwa kwa nyota huyo mwenye miaka 30 ambaye ametua hapo kwa mkopo kuwa mbadala wa Marcus Rashford ambaye anasumbuliwa na majeruhi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala