Connect with us

Makala

Bodi Ya Ligi (TPLB) Yatoa Onyo Kwa Waamuzi

Mwamuzi Florentina Zablon aliyechezesha mchezo namba 17 kati ya Mbeya City dhidi ya Yanga katika uwanja wa Sokoine amepewa onyo kali kutokana na kushindwa kutafsiri sheria licha ya uwanja kujaa maji kutokana na mvua kubwa kunyesha jijini Mbeya.

Mwamuzi Jonesi Rukya na msaidizi wake Soud Lilla nao wamepewa onyo kali baada ya kushindwa kuona baadhi ya matukio katika mchezo kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Taifa, Januari 4.

Maamuzi hayo yametangazwa mbele ya vyombo vya habari na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya ligi, Ibrahim Mwanyela katika ofisi za Shirikisho la soka Tanzania (TFF) zilizopo Karume, Dar es Salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala