Connect with us

Soka

Al-Masry Wafungiwa Miezi 18

Shirikisho la kandanda duniani FIFA, limeifungia klabu ya Al Masry ya Misri kutosajili katika madirisha matatu yajayo kwa kosa la kumsajili Cheick Moukoroo Raia wa Ivory Coast kinyume na sheria za usajili.

Taarifa kutoka Shirikisho la kandanda Misry EFA limethibitisha kupokea barua hiyo ya FIFA siku ya Jumanne ikisema “Masry imefungiwa madirisha matatu yajayo kutosajili mchezaji yeyote.” Huku barua hiyo ikieleza wazi kuwa kuanzia dirisha hili adhabu hiyo imeanza kufanya kazi. Pia Shirikisho hilo (FIFA) limetoa ofa kwa klabu hiyo kukata rufaa kuhusu adhabu hiyo. .

Moukoroo mwenye Umri wa miaka 28, tayari alikuwa akimalizia adhabu yake kutojihusisha na kandanda kwa kosa la kukatisha mkataba pasipo makubaliano na klabu yake aliyokuwepo (Al Hilal Oubeid) ya Sudan katika dirisha kubwa la usajili 2017.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka