Connect with us

Soka

Morrison Amjibu Eymael

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amesema anapofanya mbwembwe uwanjani halengi kuwadhihaki timu pinzani bali ni mahsusi kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki ambao wamelipa viingilio kuingia uwanjani

Aidha Bernard ameongeza kuwa hatafanya matukio hayo wakati wote, isipokuwa pale ambapo timu iko kwenye mazingira ya uhakika wa kuondoka na ushindi

Morrison ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kocha Luc Eymael kueleza kutofurahishwa na matukio hayo ambayo aliyafananisha na dhihaka kwa timu pinzani

“Mashabiki wanakuja uwanjani kuona timu yao inashinda, ndio maana wanalipa viingilio, lakini ninapoona timu inaongoza vizuri huwa naona ni bora kufanya kitu ambacho kitawapa burudani zaidi mashabiki wakienda nyumbani wapate cha kusimulia zaidi,” amefafanua Morrison.

“Nafikiri kocha yeyote hawezi kukubali hilo moja kwa moja, namheshimu kocha wangu (Eymael) kwa alichoniambia, lakini kwangu nafikiri kuna kitu cha ziada natakiwa kukifanya kama mchezaji, sidhani kama naweza kuacha lakini nitakuwa makini wakati gani nafanya hivyo”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka