Connect with us

Makala

Hakika Simba Ni Baba Lao

Simba imeibuka na ushindi  katika uwanja wa CCM Kirumba kwa kuwafunga Alliance Fc mabao 4-1 na kuweza kutimiza ndoto yao ya kunyakua pointi sita za kanda ya ziwa.

Alliance Fc walianza kupeleka mashambulizi kwenye lango la Simba hatimaye dakika ya 27 waliweza kupachika bao la kwanza katika nyavu za simba mkali kupitia Patrick Mwenda.

Bao la kusawazisha kwa timu ya Simba lilifungwa dakika ya 45 kupitia Jonas Mkude kabla ya kwenda kipindi cha kwanza cha mapumziko na baada ya kurudi kipindi cha pili Meddie Kagere aliongeza bao la pili kwa Simba.

Clatous Chama aliongeza furaha ya mashabiki dakika ya 63 baada ya kufunga bao la tatu kwa simba na dakika ya 72 Hassan Dilunga anakamilisha bao la nne ambalo linamfanya kocha wao mkuu Sven Vanderbroeck kujivunia kuwa na timu hiyo.

Simba ambao ni mabigwa watetezi wanafikisha jumla ya pointi 41 katika mechi 16 wakiwa wametoa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja mbele ya Mwadui Fc na kushinda mechi 13.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala