Connect with us

Makala

Fabinho Arejea Liverpool

Mchezaji wa Liverpool Fabinho arejea tena kwenye timu yake baada ya kupata tatizo kwenye enka tangu Novemba ambapo alitoka kwenye mashindano ya ligi.

Reds wamefanikiwa kufunga kila mchezo kwenye utowekaji wake isipokuwa kwenye mchezo waliocheza na Aston Villa kwenye kombe la ligi ya nusu fainali walifungwa mabao 5-0.

Kurejea kwa Fabinho kumeleta matumaini makubwa sana kwa Liverpool kwani ameripoti wiki hii kuanza mazoezi na atakuwa kwenye michezo ijayo ya ligi .

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amemkaribisha Fabinho kamili kwenye mazoezi ya wiki hii na atakuwa kiungo kwenye mechi watakayoicheza Jumapili dhidi ya Manchester United.

Fabinho amesema weekend iliyopita kuwa “Enka yangu kwa sasa ina afadhali kwa kuwa nimekuwa nikifanya mazoezi mwenyewe wiki hii nafurahi kushika mpira tena najisikia vizuri na ninajiamini”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala