Connect with us

Makala

Hao Gsm Usipime

GSM ni kampuni inayouza nguo,samani na vifaa vingine vya ndani kama makabati ,magodoro nakadhalika ukiachana Sport Pesa ambao wamekuwa ni wadhamini wakuu wa Yanga.

Kampuni hii imekuwa tofauti kidogo na wadhamini wengine kwenye klabu ya Yanga kwa ukaribu na urafiki unaoendana na undugu kwa kuwepo kipindi chote cha kutatua matatizo ya timu hiyo.

Watanzania wote wanafahamu fika Yanga ni timu ya wananchi na haijawahi kwenda sehemu kushiriki michezo ikakosa mashabiki.

Yanga imepitia  kwenye mikono mingi ya watu binafsi kama Yusuph Manji lakini kwa sasa inapaswa kuwaonyesha GSM kuwa wapo sehemu sahihi na wabakie Jangwani.

GSM imefanya vitu vingi Yanga ikiwa kutoa jezi mbili kwa kila mchezaji na vifaa vya mpira pia tumeona namna kampuni hiyo inavyoshiriki katika kuwasajili wachezaji wapya kama Juma Kotei mchezaji wa zamani wa simba pia na kocha kutoka Ubelgiji Luc Eymael.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala