Connect with us

Soka

Simba Yamtambulisha Kocha Mpya

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imemtangaza mbelgiji Sven Ludwig Vanderbroeck kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho akichukua nafasi ya Patrick Aussems aliyefungashiwa virago.

Kocha huyo amewahi kufundisha timu ya Taifa ya Zambia kuanzia julai 2018 lakini alitimuliwa miezi nane baadae baada ya kushindwa kuisaidia Zambia kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2019 zilizofanyika nchini Misri.

Kocha huyo pia alishinda Ubingwa wa Afrika (AFCON) akiwa Kocha Msaidizi za timu ya taifa ya Cameroon mwaka 2017 akimsaidia Hugo Broos.

Akiwa mchezaji amewahi kubichezea vilabu vya Mechelen, Roda JC, De Graafschap, Akratitos, Lierse, Visé na Løv-Ham kama kiungo mkabaji.
.
Anarithi mikoba ya mbelgiji mwenzake Patrick Aussems aliyetimuliwa na klabu hiyo

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka