Connect with us

Makala

Matola Atua Simba

Kocha Selemani Matola ameanza rasmi kazi ya kuifundisha timu ya Simba akiwa kama kocha msaidizi akitokea Polisi Tanzania baada ya kuvunja mkataba na timu hiyo.

Matola aliyewahi kuwa kocha msaidizi klabuni hapo miaka ya nyuma tayari ameanza kazi hiyo akichukua nafasi ya Dennis Kitambi ambaye amesitishiwa mkataba na klabu hiyo ambayo imeamua kuvunja benchi lote la ufundi lililokua likiongozwa na Patrick Aussems.

Taarifa rasmi iliyotolewa na waandishi wa habari imeonyesha pia kuwa matola atakua kocha mkuu wa timu ya vijana ya timu hiyo kama ambavyo taarifa inavyosomeka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala