Connect with us

Soka

Hans Anukia Yanga

Inaelezwa kuwa kocha Hans Van de Pluijm ametuma barua ya kuomba kurejea Yanga sc kama kocha mkuu kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha Mwinyi Zahera.

Hans aliifundisha Yanga kwa mafaniko makubwa misimu takribani mitatu hadi hapo aliopoondoka na kumpisha George Lwandamina huku akielekea Singida United ambapo hakudumu na akajiunga na Azam Fc.

Taarifa za ndani zinadai kocha huyo ameomba kurejea Yanga na yuko tayari kufanya kazi na Mkwasa kama msaidizi wake akiwa tayari walishafanya kazi hapo awali huku ikielezwa kuwa chanzo cha kocha huyo kuomba kurudi ni upendo anaoupata kutoka kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka