Connect with us

Soka

Yanga Yakomaa na Lamine

Uongozi wa klabu Yanga umesema hauna mpango wa kumuacha beki wao kisiki Lamine Moro ambaye aliandika barua ya kuvunja mkataba wake kutokana na madai ya mishahara

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amekiri beki huyo kuwa na madai ya mishahara miwili na sio mitatu

“Lamine bado ni mchezaji wetu kwani ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu. Madai yake ya mishahara ya miezi miwili pamoja na wachezaji wengine wote watalipwa leo,” amesema

Ataja sababu ya kumtema Sadney

Aidha Dk Msolla amesema uongozi umeamua kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake Sadney Urikhob kutokana na uwezo wake kutoendana na matarajio ya klabu

Dk Msolla amesema Sadney aliomba mkataba wake kuvunjwa na uongozi uliridhia kwa kuwa hakuweza kufikia matarajio ya timu

“Tumemwachia Sadney kwakuwa uwezo wake ni mdogo lakini tunapambana kumzuia Lamine Moro asiondoke. Mpira ni mchezo wa wazi , uwezo wa beki huyu kila mtu ameuona”

Habari kwa msaada wa Mitandao ya Kijamii

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka