Connect with us

Soka

Kitambi Aongoza Mazoezi Simba

Wakati kocha mkuu wa timu ya Simba sc Patrick Aussems akiendelea na adhabu kocha msaidizi wa klabu hiyo Dennis Kitambi ameongoza mazoezi asubuhi ya leo yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam.

Aussems amesimamishwa na bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa kuondoka nchini kinyume na taratibu huku akigomea kuhudhuria kikao cha kujieleza alichoitwa na uongozi bila taarifa rasmi.

Kocha huyo inadaiwa amesimamishwa mpaka novemba 28 ambapo bodi ya wakurugenzi itakaa na kutoa maamuzi ikiwa asamehewe au la huku kukiwa na taarifa za kocha huyo kukaribia kujiunga na klabu ya Polokwane city baada ya kufanya mazungumzo na bosi wa klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka