Connect with us

Soka

Mashabiki Simba sc Wamvamia Aussems

Mashabiki wa Simba sc jana walitoa kali ya kufungia mwaka baada ya kumvamia kocha Patrick Aussems ili kupiga nae picha baada ya mchezo mchezo dhidi ta Ruvu Shooting kumalizika na ushindi wa mabao 3-0 katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Mashabiki hao walimvamia kocha huyo huku wakiimba nyimbo za kumsifia wakitamka “Tunakupenda uchebe hata kama viongozi hawakutaki sisi tunakutaka na kukupenda”huku baadhi wakimvamia na kutaka kupiga picha na kocha huyo.

Polisi walifanikiwa kumpa ulinzi kocha huyo ili aweze kutoka uwanjani salama huku pia wakifanikiwa kuwadhibiti mashabiki waliokua wakitaka kupiga picha na Meddie Kagere na Tairone Dos Santos na kuwaacha mashabiki hao wakilalamika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka