Connect with us

Soka

Simba Yajichimbia Kileleni

Timu ya soka ya Simba sc imeendelea kusimama kileleni mwa ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting  jioni ya leo katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulionza kwa kasi huku Simba ambao walikua wageni siku ya leo wakishambulia lango kwa kasi japo walikosa nafasi kadhaa za kufunga mpaka dakika ya 40  ambapo staa anayekuja juu katika timu hiyo Miraji Athuman alipofunga bao la kwanza lililodumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili Simba iliandika bao la pili kupitia kwa  Mbrazil Tairone Santos aliyemalizia kona ya Francis Kahata kabla ya Miraji kupachika bao la tatu na la ushindi akimalizia pasi ya Kahata dakika ya 75.

Simba imefikisha jumla ya alama 25 na kukaa kileleni mwa ligi hiyo huku ikiwa imecheza michezo kumi na kufunga mabao 23.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka