Connect with us

Makala

Tetesi za Usajili Ulaya

Meneja mpya wa Tottenham Jose Mourinho atajaribu kumsajili tena mshambuliaji wa zamani wa Spurs Gareth Bale, 30, kutoka Real Madrid. (AS – in Spanish)

Mourinho pia anamlenga kiungo wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 25, mlinzi wa kati wa Benfica Mreno Ruben Dias, 22, na kiungo wa kati wa Manchester United Mserbia Nemanja Matic, 31. (Independent)

Mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, 27, na mlinzi wa kushoto wa raia wa Scotland Andrew Robertson, 25, watakosa mechi ya Liverpool dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi.(Sky Sports)

Juventus inatarajiwa kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kupuuzilia mbali Real Madrid na kujiunga na klabu hiyo ya Serie A kutoka Paris St-Germain. (Tuttosport, via Sky Sports)

Mlinzi wa zamani wa Arsenal Martin Keown anaamini kuwa Gunners inahitaji kumuajiri meneja wa zamani Tottenham, Mauricio Pochettino. (Mail)

Barcelona na Bayern Munich ziko tayari kumpatia kazi Mauricio Pochettino. (Sun)

Mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, bado hajasaini mkataba mpya na Arsenal kwa sababu anasubiri uamuzi wa Barcelona. (Mirror)

Real Madrid imemuunga mkono Bale na kupuuzilia mbali tetesi kuwa nyota huyo huenda akaondoka klabu hiyo mwezi Januari. (Marca)

Manchester United inatafakari uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Roma wa miaka 33, mzaliwa wa Boznia, Edin Dzeko. (ESPN)

Wakala wa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, Mino Raiola amekutana na AC Milan kuhusu uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Sweden kurejea katika klabu hiyo. (Corriere dello Sport – in Italian)

Mpango wa Inter Milan wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, huenda ukatibuliwa na matakwa ya mchezaji huyo. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)

Chelsea imeungana na Liverpool na Napoli katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Genk na Norway, Sander Berge,21. (goal)

Kiungo wa kati wa England, James Maddison, 22, anajiandaa kusaini mkataba mpya na Leicester licha ya azma kuu ya Manchester United ya kutaka kumnunua. (Manchester Evening News)

Arsenal na Liverpool zimehusishwa na tetesi ya usajili wa mshambuliaji wa Red Bull Salzburg ya Ujerumani Karim Adeyemi,17. (Transfermarkt, via HITC)

Arsenal imeongeza juhudi za kumnunua mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland, 19, baada ya kumwalika baba ya mchezaji huyo, Alf-Inge Haaland ambaye alikuwa kiungo wa kati wa zamani wa Leeds, kutembelea uwanja wao wa mazoezi. (Sport Bild, via Metro)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer pia anapania kumsaini Haaland. (Mail)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala