Connect with us

Soka

Lamine Bado sana

Wakati nyota waliokuwa majeruhi wakirejea kikosini, beki Lamine Moro bado anaendelea na matibabu ambapo aliumia katika mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc, mchezo ambao Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0

Kaimu kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema bado hajafahamu ni wakati gani beki huyo kisiki atarejea kikosini “Wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea kikosini isipokuwa wachezaji wawili, Lamine Moro na Maybin Kalengo,” alisema Mkwasa jana baada ya mazoezi “Sina hakika ni wakati gani watarejea lakini jambo la msingi ni kwamba wachezaji waliopo wataweza kutusaidia”

Kalengo inafahamika atarejea kikosi mwakani baada ya kupata majeraha makubwa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba Fc jijini Mwanza

Katika mazoezi ya jana, idadi kubwa ya wachezaji waliokuwa majeruhi walishiriki

Wachezaji hao ni pamoja na Sadney Urikhob, Juma Balinya, Mohammed Issa ‘Banka’,Ally Ally na Paulo Godfrey ‘Boxer’

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka