Connect with us

Soka

Stars Yapaa,Nyoni Abaki

Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa stars) imekwea pipa leo alfajiri kuelekea nchini Tunisia kucheza mechi ya pili ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Libya itakayofanyika siku ya jumanne nchini Tunisia.

Stars imekwenda nchini humo kufuatia hali ya usalama nchini Libya kuwa finyu hivyo kulazimisha shirikisho la soka barani Afrika kuhamishia mchezo huo nchini Tunisia.

Stars imesafiri bila ya kiraka Erasto Nyoni ambaye anasumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata jana wakati wa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Equatorial Guinnea na hivyo kubakishwa nchini kwa uangalizi zaidi.

“Erasto Nyoni ameshindwa kusafiri sababu alipata majeraha ya goti jana, naamini tutapata mchezaji sahihi wa kucheza eneo lake.”Alisema kocha Ettiene Ndayiragije wakati akihojiwa na vyombo vya habari.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka