Connect with us

Soka

Kante Akomaa Darajani

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 28, amekana taarifa zinanazomuhusisha na kuhamia katika klabu ya Real Madrid na anasema kuwa anaweza kumalizia taaluma yake ya soka katika Stamford Bridge.

Kwa kweli, natarajia kumaliza kazi yangu Chelsea.” alisema Kante akihojiwa katika mahojihano na “Telefoot”.

“Leo nipo na Chelsea hadi 2023. Kwa hiyo kichwani kwangu, natumaini kuendelea kuwa na misimu mizuri na Chelsea hadi 2023.” .
.
Alipoulizwa kuhusu tetesi zinazo muhusu kuhamia Real Madrid, majibu ya Kante yalikuwa rahisi tu “Hapana, sio kweli”

Kante alijiunga na Chelsea akitokea Leicester city baada ya kuwa ameisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza na mpaka sasa amekua mhimili katika kikosi hicho japo amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka