Connect with us

Soka

Majanga Chelsea

Kocha Frank Lampard ana kazi kubwa ya kuhakikisha anaibuka na ushindi katika michezo ya ligi kuu nchini humo huku akikabiliwa na majeruhi hasa ya wachezaji muhimu kikosini humo.

Lampard atawakosa beki kisiki Antonio Rudiger huku pia akimkosa Ross Barkley baada ya wote kupata majeraha huku Rudiger akiwa amejitonesha baada ya kuwa ameanza mazoezi akitoka kufanyiwa upasuaji wa mguu.

Ross Barkley akipewa siku kumi za mapumziko kufuatia kuwa majeraha na Kiungo Mason Mount akiwa na hatihati mpaka uchunguzi wa kina kuhusu afya yake ufanyike.

Ruben Loftus Cheek naye yupo kitandani akijiuguza na maumivu ya kiwiko aliyopata wakati akiitumikia klabu hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka