Connect with us

Soka

Kmc Watimua Kocha

Timu ya soka ya manispaa ya Kinondoni(Kmc) imemtimua kocha Jackson Mayanja baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha hasa uwanjani hususani baada ya kutopata matokeo yasiyorodhisha.

Timu hiyo imekua na mwenendo wa kusuasua tangu ilipoachana na kocha Ettiene Nadyiragije ambaye alijiunga na Azam fc kisha taifa stars ndipo alipoteuliwa mayanja kushika nafasi hiyo na licha ya kutofanikiwa kuingia raundi ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kutolewa na As kigali ya Rwanda bado aliendelea kupoteza michezo ya ligi kuu ikwemo wa jana dhidi ya Kagera Sugar.

Taarifa rasmi kutoka Kmc imeeleza kuachana na kocha huyo baada ya makubaliano ya pande mbili kufikiwa kwa maslahi mapana ya klabu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka