Connect with us

Soka

Prisons Wamkomalia Mnyama Taifa

Timu ya Prisons imefanikiwa kulazimisha suluhu na Simba sc katika mchezo uliomalizika jioni hii katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

Mchezo ulioanza kwa kasi ukitawaliwa na krosi nyingi kuelekea langoni mwa Prisons ulimalizika kwa matokeo hayo baada ya mabeki wa timu hiyo kufanikiwa kuwadhibiti Meddie Kagere na Miraji Athuman huku Cletous Chama na Shiboub wakikosa ubunifu wa kupenyeza mpira langoni mwa wajelajela hao.

Kwa matokeo hayo bado Simba wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 22 huku prisons akipanda mpaka nafasi ya pili akiwa na pointi 19 baada ya kucheza michezo 11.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka