Connect with us

Soka

Azam, Kagera Hakuna Mbabe

Klabu ya Azam Fc imetoa suluhu na timu ya Kagera sugar katika mchezo wa ligi kuu ya nchini uliochezwa katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam.

Wenyeji walijitahidi kutafuta nafasi za kupata goli lakini walishindwa kutokana na uimara wa beki Juma Nyoso huku Donald Ngoma akikosa nafasi kadhaa za wazi hasa alipobaki na golikipa pekee lakini alishindwa kuipatia bao timu yake.

Azam imeambulia pointi moja katika michezo miwili ambayo kocha Aristica Cioaba amekaa benchi baada ya kufungwa na Ruvu Shooting na jana kutoa Sare.

Matokeo haya yanaifanya Azam FC kuwa nafasi ya 14 ikiwa na pointi zake 10 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya pili ina pointi 17 baada ya kucheza mechi 9 huku Simba akiongoza ligi kwa pointi 21 katika michezo nane.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka