Connect with us

Soka

Kadi Zawaponza Mastaa Alliance

Uongozi wa timu ya Alliance FC kutoka mkoani Mwanza, umeomba radhi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyofanywa na wachezaji wao wawili Israel Patrick na John Mwanda katika mchezo wao na Mbeya City uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo Yusuph Budodi amesema wamesikitishwa na vitendo hivyo na kama uongozi hawawezi kuvivumilia hivyo watachukua uamuzi stahiki baada ya kamati ya nidhamu ya klabu hiyo kukaa na wachezaji hao kuwasikiliza.

“Uongozi wa Alliance FC umewaita wachezaji hao wawili leo na shauri lao limepelekwa Kamati ya Nidhamu” amesema Yusuph Budodi.

Kwenye mchezo huo, wachezaji Israel Patrick Mwenda ambaye ni nahodha wa timu ya Alliance FC alipewa kadi nyekundu baada ya kuonekana akimshika sehemu za siri mchezaji wa Mbeya City George Chota huku kipa John Mwanda naye akipata kadi nyekundu kwa kumpiga mtama mchezaji wa Mbeya City Idd Gamba.

Wachezaji hao wawili wamepewa barua za kuitwa kwenye Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Alliance FC kesho saa nne asubuhi kwa hatua zaidi.

Habari kwa msaada wa Azam Tv.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka