Connect with us

Soka

Zahera Matatani

Kufuatia kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Pyramids Fc kocha wa timu ya Yanga sc Mwinyi Zahera ameingia matatani baada ya mashabiki wa klabu hiyo kumtaka ajiuzuru baada ya kutopata matokeo waliyoyatarajia katika mchezo huo uliofanyika jijini Mwanza.

Zahera anashutimiwa na mashabiki kutokana na mbinu zake katika mchezp huo ambapo alijaza viungo wengi na kuacha mshambuliaji mmoja pekee ambaye alishindwa kufurukuta katika mchezo huo.

Mabao ya Pyramids yalipatikana kutokana na mbinu hiyo ya Zahera kutofungua uwanja huku baadae alipobadilisha mbinu kwa kuwaingiza Patrick Sibomana na Juma Balinya na kusababisha kupata bao dakika za mwishoni lililofungwa na Tshitshimbi.

Mashabiki walimzomea na kumpiga chupa kocha huyo wakimshinikiza ajiuzuru huku wakiimba nyimbo za kumtaka aondoke.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka