Connect with us

Soka

Sadney Amaliza Mchezo Kirumba

Mshambuliaji Mnamibia wa klabu ya Yanga hatimaye amefunga goli lililoipa klabu yake ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao Fc katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

Mbao licha ya kuwa nyumbani wamekubali kipigo hicho baada ya kuruhusu goli dakika ya 62 baada ya mabeki wa timu hiyo kushindwa kuokoa krosi ya Balama Mapinduzi aliyekua mwiba katika mchezo wa leo.

Yanga walijitahidi kupeleka mashambulizi langoni kwa mbao ambapo umakini mdogo wa Molinga na Sadney uliwakosesha mabao kadhaa licha ya Molinga kupata nafasi za kupiga mipira ya faulo.

Kwa ushindi huo Yanga imefikisha alama saba baada ya kucheza michezo minne na itashuka tena dimbani hapo kuwakabili Pyramids Fc katika mchezo wa ligi ya kuwania kufuzu makundi kombe la shirikisho barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka