Connect with us

Soka

Yanga Kutua Mwanza Kibabe

Wakati kikosi cha timu ya Yanga kikitarajiwa kuwasili jijini humo leo ijumaa uongozi wa matawi ya timu hiyo jijini humo umewaandalia mapokezi ya kibabe mabingwa hao wa kihistoria nchini.

Yanga wanatua jijini humo kuweka kambi ya muda kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya mbao na Alliance huku pia wakiwa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Pyramids fc ya nchini Misri ambao utafanyika jijini humo katika uwanja wa Ccm Kirumba.

Uongozi wa matawi hayo umethibitisha kuandaa mapokezi hayo kwa mujibu wa katibu mkuu Mhando Madega “Tulikuwa na kikao na viongozi wa matawi ya Yanga jijini Mwanza kwa pamoja tumeazimia kuipokea timu yetu kwa mapokezi makubwa ikiwa ni ishara ya kufanya vyema katika michezo yetu miwili dhidi ya Mbao na Pyramids.

Yanga inatakiwa kushinda michezo hiyo ya ligi ili kuongeza idadi ya pointi na kujiwekea mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu huku pia ikiwa na kibarua cha kuhakikisha inapata matokeo dhidi ya Pyramids ili kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka