Connect with us

Soka

Stars Yatua Sudan

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) imewasili mjini Khartoum nchini Sudan kuelekea mchezo wa kimataifa wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) ikitokea Kigali Rwanda ilipokwenda kucheza mchezo wa kirafiki.

Baada ya mchezo huo na The amavubi ambao uliisha kwa suluhu Stars ilipaa mpaka jijini Khartoumu kuwahi maandalizi ya mwisho katika mchezo huo wa marejeano ambapo mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam uliisha kwa Stars kufungwa 1-0.

Ili ifuzu Stars inahitaji kufunga mabao kuanzia mawili huku isiruhusu kufungwa mabao mengi ili kuwa na tofauti ya mabao ya ugenini na nyumbani ili kupata nafasi hiyo ya kushiriki fainali hizo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka