Connect with us

Makala

Yanga Yaangukia Uarabuni

Klabu ya Yanga sc imepangwa kucheza na timu ya Pyramid fc ya nchini Misri katika droo ya michuano ya kombe la shirikisho iliyofanyika jana kwa hatua za mtoano ili kufuzu hatua ya makundi.

Yanga itakabiliwa na mtihani mgumu dhidi ya timu hiyo ambayo ina kikosi chenye thamani ya zaidi ya bilioni 50 huku ikiwa na wachezaji ghali akiwemo staa wa Brazil Keno aliyesajiliwa kutoka Palmeiras kwa gharama ya zaidi ya bilioni 20.

Wanajangwani hao wataanzia nyumbani oktoba 27 mwaka huu na kisha watakwenda kwenye mechi ya marudiano nchini Misri itakayofanyika Novemba 3 na endapo wataibuka na ushindi wa jumla katika mechi hizo basi watafuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Pyramids Fc ilianzishwa mwaka 2008 huku ikitumia uwanja na 30 june kama uwanja wa nyumbani wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 30000 huku mmiliki wa klabu hiyo Salem Al Shamsi aliyeinunua mwaka huu mwezi julai huku ikifundishwa na aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Uganda Sebastien Desabre.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala