Connect with us

Soka

Yanga Yashtakiwa Tff

Klabu ya Yanga imeshtakiwa katika kamati ya katiba,sheria na haki za wachezaji iliyopo ndani ya shirikisho la soka nchini kufuatia kushindwa kulipa madai ya wachezaji Pato Ngonyani,Matheo Anthony na Haji Mwinyi Mngwali ambao waliitumikia klabu hiyo misimu kadhaa iliyopita.

Wachezaaji hao kwa pamoja walifikisha malalamiko yao katika chama cha wachezaji(Sputanza) ambacho kiliamua kuchukua hatua ya kuripoti suala hilo kwa kuandika barua kwa katibu mkuu wa Tff Wilfred Kidao ili afikishe suala hilo kwa kamati hiyo huku klabu ya Yanga nao wakiandikiwa barua kuhusu madai ya wachezaji hao.

“Naidai yanga fedha nyingi sana zaidi ya shilingi milioni kumi ambazo ni fedha za usajili na malimbikizo ya mishahara ya miezi zaidi ya mitatu”Alisema Pato anayeichezea timu ya Polisi Tanzania.

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alikiri kudaiwa na wachezaji wengi madeni ambayo aliyakuta klabuni hapo kutokana na klabu hiyo kukabiliwa na ukata msimu uliopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka