Connect with us

Soka

Hali Tete Tottenham

Licha ya dirisha la usajili kufungwa bado bundi ametanda katika klabu ya Tottenham kufuatia mastaa kibao kumaliza mikataba yao mwakani hivyo kuanzia januari watakua huru kuzungumza na klabu zingine.

Mastaa kama Christian Ericksen ambaye alitaka kuondoka dirisha la kiangazi kujiunga na Real Madrid japo usajili ulishindikani lakini unaweza kufanyika mwakani huku Toby Alderweireld na Dany Rose wakiwa na mipango kama hiyo na sasa Jan Vertogen nae amegomea mkataba mpya na kuleta sintofahamu.

Mkanganyiko huo umeleta matokea hasi uwanjani ambapo timu hiyo imetolewa katika mashindano ya Carabao cup baada ya kufungwa na timu ya Colchester inayocheza madaraja ya chini nchini humo pia katika ligi kuu imecheza mechi sita ikishinda mbili,droo mbili na kufungwa mbili na kubaki nafasi ya nane.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka