Connect with us

Soka

Messi Aipasua Kichwa Barca

Staa wa Barcelona Lionel Messi ameipasua kichwa klabu hiyo baada ya kucheza dakika 45 tu kisha kuumia kwa mara nyingine katika mchezo wa jana dhidi ya Villareal mchezo wa ligi kuu nchini Hispania(La liga).

Messi aliyetoka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume duniani hakuichezea timu hiyo toka mwanzoni mwa msimu huu kutokana na kusumbuliwa na kiwiko cha mguu wake hali iliyosababisha staa huyo kutocheza mechi yeyote msimu huu.

Katika mchezo huo Barcelona ilishinda 2-1 kwa mabao ya Antoine Griezmann dakika ya 6 na Athur Mello dakika ya 15 nakuwafanya kupanda mpaka nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo maarufu duniani wakiwa wamejikusanyia pointi 10 baada ya kushinda michezo mitatu huku wakipoteza mmoja na kutoa sare mmoja.

Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde amesisitiza kumhitaji mechi kabla ya jumamosi kwenye mechi dhidi ya Getafe na wiki ijayo watakapowavaa Intermilan kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka